UONGOZI WA CHUO CHA ARDHI MOROGORO (ARIMO) UNATANGAZA KWA MASIKITIKO MAKUBWA KIFO CHA MKUFUNZI MKUU, BW. STANLEY ELIEZER, KILICHOTOKEA USIKU WA LEO, TAREHE 5 DESEMBA 2024.
MSIBA HUU NI PIGO KUBWA KWA FAMILIA YAKE, WANAJUMUIYA WA ARIMO, NA WOTE WALIOMFAHAMU KWA MCHANGO WAKE MKUBWA KATIKA SEKTA YA ELIMU NA MAENDELEO YA NCHI YETU.
MIPANGO YA MAZISHI INAENDELEA KUFANYIKA CHUONI MOROGORO, NA TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KADRI MAANDALIZI YANAVYOENDELEA.
UONGOZI WA CHUO CHA ARDHI MOROGORO UNATOA POLE NYINGI KWA FAMILIA, WANAJUMUIYA WA ARIMO, NDUGU, JAMAA, NA MARAFIKI WOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUU MZITO.
BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
IMETOLEWA NA:
UONGOZI WA CHUO CHA ARDHI MOROGORO (ARIMO)